Thursday, August 20, 2009

MKUU WA WILAYA KINONDONI AANZA KUTENGENEZA TIMU YA KUFANYA KAZI KINDOZIMh. Lugimbana mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa tarehe 18/08/2009 hadi 19/08/2009 alikuwa na kikao cha kazi kati ya Maafisa Watendaji wa Kata zote 27 za Manispaa ya Kinondoni, Maafisa Watendaji Wamitaa katika mitaa yote 127 ya Manispaa ya Kinondoni na Maafisa Afya wa Manispaa ya Kinondoni.
Semina hii iliandaliwa na Kamati ya Usafi ya Manispaa ya Kinondoni ikiongozwa na Mh. DC Lugimbana kwa lengo la kuliandaa jeshi la kuweza kupambana na hali ya uchafu katika Manispaa yetu ya Kinondoni pamoja na kero nyingine zinazowahusu wananchi wa Manispaa ya Kinondoni.
Kikao hiki cha kazi kiliwahusisha pia vyombo vya usalama - Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni chini ya RSO, DSO's wake, pia RPC na OCD's wa mkoa wa Kinondoni.Lengo la msingi ni kuwawezesha watendaji kwanza kujenga mahusiano na viongozi hao na pia kushirikiana katika mbinu mbalimbali za utendaji wa kazi zetu.
Mambo yalikuwa mazuri embu endelea na kujionea mambo yalivyokuwa:-
No comments: